Articles

LIPSTICK KWA WAJAWAZITO

By

on

Mjamzito

Lipstick

Lipsticks

 

Kipodozi ni kitu ambacho mtu anakitumia katika mwili wake ili kubadilisha muonekana wa mwili wake na kumfanya apendeze au aonekane tofauti na ilivyo asili ya mwili wake.

Yawezekana kipodozi kikatumika kubadili muonekano wa nywele kichwani, kope za macho, midomo (lips), kucha na hata ngozi ya mtu. Miongoni mwa vipodozi ambavyo ni maarufu na vinatumiwa na watu wengi ni, lipstick.

Lipstick ni aina ya kipodozi ambacho kimetengenezwa kutokana na mchanganyiko wa nta (waxes), mafuta, rangi mbalimbali (pigments) pamoja na metali (metals) tofauti tofauti na hutumika kwa kupakwa katika midomo (lips) ili kuzifanya lips ziwe na mng’ao, ziwe na unyevu (moisture) na pia ulinzi (lips protection).

Kama ambavyo sote tunafahamu kuwa, wajawazito ni kundi pekee sana katika jamii, kwa maana ya kwamba ni watu wanaohitaji kuwa waangalifu au kuwa nao karibu sana na kuhakikisha kuwa, kila wanachokitumia ni salama kwa mama mwenyewe na pia kwa kiumbe kilichopo tumboni, hii ni uangalifu katika chakula wanachokula, vinywaji, dawa, mavazi, vipodozi/urembo na vingine vingi.

Siyo vibaya kwa mama mjamzito kujiweka katika hali ya kupendeza kwa kutumia kipodozi, lakini swali la msingi ni kwamba, je kipodozi anachokitumia ni salama kiasi gani kwake yeye na pia kwa mtoto aliyeko tumboni?.

Tafiti zinaonyesha kuwa, lipstick nyingi zinamchanganyika wa metali (metals) ambazo zinaboresha muonekana wa lipstick lakini usalama wake kwa mtumiaji siyo wa kutosha. Moja ya metali hizo ni risasi (lead). Baada ya kutumia lipstick yeyote ile, utakubaliana na mimi kuwa, kuna kiasi ambacho kwa namna moja au nyingine kitaingia mwilini mwako kwa njia ya kula pamoja na chakula, vinywaji na hata baadhi kitaingia mwilini kwa kupenyeza katika ngozi yako.

Endapo metali hii ya risasi (lead) itaingia mwilini, inaleta madhara kiafya ambayo kwa mama mjamzito huweza kupelekea kuathiri ukuaji wa ubongo wa mtoto, figo, mfumo wa fahamu, tabia ya mtoto na pia hupelekea mama mjamzito mimba ikatoka au kujifungua mtoto kabla ya siku zake kufika.

Yawekenana ukiwa mjamzito, unao ulazima wa kutumia kipodozi/urembo, jambo ambalo tunapaswa kukumbuka ni kusoma taarifa (labels) katika kile tunacho kichagua, je kina mchanganyiko ambao ni salama kwangu mimi na mtoto niliyenaye tumboni?. Kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza madhara ya kiafya yanayotokana na utumiaji wa vitu visivyohitajika katika miili yetu.

‘Mtu wa kwanza mwenye wajibu wa kuilinda afya yako, ni wewe mwenyewe’

Chanzo: Tanzlife Company Limited

About Admin

Avatar

Recommended for you

3 Comments