Articles

JE, TAARIFA UNAYOPASWA KUMPATIA MGONJWA/MTAALAMU WA AFYA, UNAMPATIA?

By

on

MAWASILIANO KATI YA MTOA NA MPEWA HUDUMA YA AFYA

MAWASILIANO KATI YA MTOA NA MPEWA HUDUMA YA AFYA

Lengo la mada hii ni kukumbushana na kubadilishana mawazo juu ya uhusiano au mawasiliano kati ya watoa huduma za afya pamoja na wapewa huduma za afya (wagonjwa). Siyo mara moja imetokea mtu akatoka kwa daktari wake kupewa huduma lakini ukimuuliza unatatizo gani, akakujibu mimi nimeambiwa nitumie dawa hizi (hajui tatizo lake), au mtu katoka kupewa dawa za kutumia lakini ukimuuliza dawa hizi unatumiaje, akakujibu nimeambiwa kutwa mara mbili, au mgonjwa unaulizwa kuna dawa zozote ulizokuwa unatumia kabla ya leo kufika hapa, anakujibu hapana (Kumbe kuna dawa alikuwa anatumia ila anataka kuona kama utamshauri atumie dawa za aina ile aliyokuwa anatumia hapo kabla).

Tatizo la mawasiliano baina ya watoa huduma na wapewa huduma za afya, huchangia mtu (mgonjwa) kutojitambua vyema afya yake, kutumia dawa visivyo sahihi, watu kupata aleji (kutumia dawa isiyo sahihi) na matatizo mengine mengi.

Wewe kama mdau (Mtoa huduma au mpewa/unayeweza kupewa huduma za afya) maoni yako ni nini juu ya changamoto hii katika huduma za afya?.

Unaweza kuchangia/kutoa maoni kupitia page hii sehemu ya maoni (Comment), kwa ku LIKE page yetu ya Facebook (Tanzlife), Twitter (@tanzlife) na pia kwa kujiunga katika Health Forum yetu katika Website ya Tanzlife na kutoa maoni yako.

BADILIKA SASA!!!

Chanzo: Tanzlife Company Limited

About Admin

Avatar

Recommended for you

2 Comments