Articles

WAJAWAZITO WATAKIWA KUJIFUNGULIA MAENEO WANAKOTOKA

By

on

HOSPITALI YA AMANA

HOSPITALI YA AMANA

Wanawake wajawazito katika Manispaa ya Ilala wameshauriwa kwenda kupata huduma katika hospitali na vituo vilivyoko maeneo yao ili hospitali ya Amana ibaki kama hospitali ya Rufaa.

Kumekuwa na msongamano mkubwa katika hospitali ya Amana kutokana  na watu wengi kukimbilia hospitali hiyo hasa kina mama wajawazito licha ya kuwepo kwa hospitali na vituo vinavyotoa huduma ya kuzalisha katika maeneo mengine ya Manispaa ya Ilala.

Meya wa Manispaa hiyo, Jerry Slaa, alisema hospitali ya Amana imekuwa ikikabiliwa na msongamano mkubwa hasa katika wodi za wazazi kutokana na wanawake wengi kukimbilia hapo licha ya kuwepo na huduma za uzalishaji katika vituo na zahanati zilizoko katika maeneo wanakotoka.

Kwa mujibu wa Meya huyo, hospitali ya Amana ilipandishwa hadhi na kuwa ya Rufaa ili kutoa nafasi kwa magonjwa ambayo yameshindikana katika zanahati, vituo na hospitali nyingine zilizoko katika Manispaa hiyo kutibiwa Amana.

Kwa mujibu wa Muuguzi Mkuu wa hospitali hiyo Agnes Mwanga, kwa siku hospitali hiyo inazalisha kina mama 100 hadi 120 huku wengine wakiwa wanatoka nje ya Manispaa hiyo.

Katika hatua nyingine, Meya huyo alisema wana mpango wa kujenga kituo kikubwa cha afya kitakachotoa tiba kwa haraka na kwa malipo.

Alisema kituo hicho kitakuwa ni cha pili kwa ukubwa katika Afrika ambapo cha kwanza kiko Lesotho.

Alisema kituo hicho kitajengwa jirani na hospitali ya Amana na kwamba kinatarajiwa kukamilika kabla ya mwaka 2015.

Chanzo: Tanzlife Company Limited

About Admin

Avatar

Recommended for you