Articles

KUWA NA MALARIA BAADA YA KUMALIZA DOZI YA MALARIA

By

on

Malaria ni ugonjwa hatari unaoenezwa kwa njia ya kung’atwa na mbu ambaye amebeba vijidudu vinavyosababisha malaria vijulikanavyo kwa jina la Plasmodium malariae.

Pamoja na kuwepo dawa mbalimbali za kupambana na ugonjwa huu, bado athari zake ni kubwa katika jamii. Watu wengi wamepoteza maisha na pia kiuchumi mtu binafsi na Taifa kwa ujumla linatumia pesa nyingi ili kudhibiti ugonjwa huu.

Katika mada hii ya leo, “Kuwa na malaria baada ya kumaliza dozi ya malaria”, nimeona ni vyema tukabadilishana mawazo juu ya tatizo hili, kwani ni watu wengi sana wamekuwa wakisumbuka na kulalamika juu ya tatizo hili. Mtu amegundulika kuwa anavyo vijidudu vya malaria, akaandikiwa atumie dawa fulani, lakini baada ya kumaliza dozi ndani ya siku tatu akipima tena anaambiwa mwilini bado anavyo hivi vijidudu vya malaria.

Je, tatizo hili linasababishwa na nini, je tatizo liko kwenye dawa, au ni namna sisi wenyewe tunavyoitumia dawa, au tatizo ni vijidudu vya malaria jinsi vilivyo au tatizo ni nini?

Tunakuomba utoe ushauri wako ili watu wengine waweze kufaidika kwani ugonjwa huu unaweza kumpata mtu yeyote hii leo, kesho na hata siku za usoni.

Unaweza kutoa maoni/ushauri wako kupitia ukurasa huu sehemu ya maoni (Comments), ukurasa wa Facebook Tanzlife, Twitter, @tanzlife, au kwa kujiunga katika Health Forum katika Website hii ya Tanzlife.

TUNAWASHUKURU KWA USHIRIKIANO

Chanzo: Tanzlife Company Limited

About Admin

Avatar

Recommended for you