Articles

MATATIZO YATOKANAYO NA KUANGALIA RUNINGA KWA MUDA MREFU

By

on

KUANGALIA RUNINGA

KUANGALIA RUNINGA

Runinga ni chombo ambacho tunakitumia katika maisha yetu ya kila siku, kwani kupitia runinga tunapata habari na pia ni njia moja wapo ya mtu kuweza kupumzika na akapata burudani.

Mpenzi msomaji, utakubaliana na mimi kwamba, kila jambo au kitu kinapokuwa kinafanyika kwa kupita kiasi, basi huwa na madhara, every thing too much, is harmful. Vivyo hivyo, kutizama runinga kupita kiasi huwa na madhara.

Tafiti mbalimbali zimefanywa na wataalamu wa afya ( chuo kikuu cha Maastricht nchini Uholanzi ) hususani katika magonjwa mbali mbali ambayo binadamu wanakuwa nayo, na kutafuta kama yana uhusiano wowote na aina ya maisha ambayo mtu anaishi au vitu ambavyo anavitumia visivyokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na mwili wake, mfano runinga. Matokea ya tafiti hizo yamebaini kuwepo kwa madhara yafuatayo ya kiafya endapo mtu atatumia muda mwingi kukaa akitizama runinga:

Kwa mujibu wa tafiti hizo, imegundulika kuwa vijana wanapotumia muda mwingi kukaa na kuangalia runinga, mishipa yao ya damu, arteries, ndivyo inavyozidi kuwa migumu (stiff arteries) na kupelekea ukubwani zaidi kuwa hatarini kupata magonjwa ya moyo.

Uchunguzi ulionyesha kuwa, watu waliotumia muda mwingi kwa siku kuangalia runinga, mishipa yao mikuu ya damu katika shingo na kichwa, Carotid Artery, ilikuwa ni migumu ( Stiff ) zaidi ukilinganisha na wale ambao walitumia muda mchache wakiangalia runinga, waliotumia muda mchache kuangalia runinga, mishipa hii kwao ilionekana kuwa laini, elastic. Pia matokea ya aina hii yalionekana katika mishipa ya damu katika miguu, femoral arteries.

Jambo ya mishipa kuwa migumu limehusishwa na uhalisia kwamba, mtu anapokaa akitizama runinga basi, ni mara chache ataamka na kujishughulisha au kuuchangamsha mwili kwa kazi na hivyo kujikuta anamaisha ya kukaa sehemu moja, sedentary lifestyle.

Matatizo yanayompata kijana katika umri mdogo ya mishipa kuwa migumu, imeonekana kuwa ni vigumu kuyaondoa pindi anapokuwa mtu mzima, hivyo yanakuwa ni matatizo ya kudumu ambayo hatari yake kubwa ni magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.

Mpenzi msomaji, kuangalia runinga siyo jambo baya, ila kutumia muda mwingi kukaa sehemu moja, siyo jambo zuri kwa afya yako. Ushauri uliotolewa na watafiti hao ni, mtu kuepuka maisha ya kukaa sehemu moja kwa muda mrefu bila ya kuushughulisha mwili. Imependekezwa kufanya mazoezi, mfano ambayo utatumia dakika 150 kwa wiki sawa na nusu saa kwa siku, ( Siku tano za wiki ), pia imeshauriwa ulaji mzuri kiafya ili kuendelea kuitunza afya.

Chanzo: Tanzlife Company Limited

 

 

 

About Admin

Avatar

Recommended for you