Articles

ALAMA ZA MICHIRIZI KWENYE NGOZI (STRETCH MARKS)

By

on

ALAMA ZA MICHIRIZI KWENYE PAJA

ALAMA ZA MICHIRIZI KWENYE PAJA

Katika ngozi ya baadhi ya watu, kuna aina Fulani ya mistari ambayo huonekana kama alama iliyobaki baada ya mtu kuumia, huonekana kama kovu, lakini siyo kovu na wala mtu hakupata ajari au kuumizwa na kitu chochote.

Mara nyingi alama hizi za michirizi humtokea mtu maeneo ambayo kwa asilimia kubwa huwa na mafuta (fat), mfano katika mwili hutokea mara nyingi kwenye mapaja, upande wa juu wa mikono (biceps), tumboni, kwenye makalio, pia kwa baadhi ya watu hutokea maeneo ya kifuani au kwenye matiti kwa wanawake.

Mpenzi msomaji, kwa kawaida michirizi hii huwa haimletei mtu maumivu ya aina yoyote, bali jambo kubwa huwa ni kuubadili muonekano wa ngozi ya mtu. Kwa baadhi ya watu michirizi hii huwa ni mikubwa sana, na kwa namna moja au nyingine humnyima mtu uhuru au humfanya mtu asiwe na amani pindi anapokuwa mbele za watu kwa kutegemeana na michirizi hiyo imetokea sehemu gani ya mwili.

Kabla hatujaangalia namna alama hizi zinavyotokea, tukumbushane sehemu muhimu za ngozi. Ngozi imegawanyika katika sehemu kuu tatu, sehemu ya nje (Epidermis), sehemu ya kati (Dermis) na sehemu ya ndani (Hypodermis).

Alama hutokea baada ya sehemu ya kati ya ngozi, dermis, kutanuka ghafla ndani ya muda mfupi kutokana na vitu kama mazoezi makali (kunyanyua vitu vizito), mtu kuongezeka uzito ghafla au obesity, pia kuna baadhi ya dawa au homoni (Glucocorticoids), ambazo kwa namna moja au nyingine huathiri tishu za kwenye ngozi na hivyo kupelekea mtu akapata alama za michirizi. Ujauzito kwa baadhi ya wanawake na pia mambo ya kurithi yameonekana kuchangia mtu kupata alama hizi katika ngozi yake.

Yawezekana alama hizi ni kero katika ngozi yako, miongoni mwa njia ambazo zinatumika kutatua au kupunguza ukali wa muonekano wa alama hizi ni: Kwanza kabisa mpenzi msomaji, ni kuangalia chanzo ni nini, je ni uzito kuongezeka ghafla?, na baada ya kugundua chanzo, chukua hatua zinazostahili, na kama chanzo ni mazoezi au kunyanyua vitu vizito, ongea na mwalimu wako wa mazoezi ili akupangie utaratibu mzuri wa mazoezi. Pia matumizi ya mafuta ya kujipakaa yenye mchanganyiko wa vitamini E husaidia kuijenga ngozi na kutoa makovu na michirizi. Ulaji wa vyakula na kunywa vinywaji vyenye vitamini A, D na E huimarisha ngozi.

Tumia vipande vidogo vidogo vya viazi kufuta sehemu ya ngozi yenye michirizi, ruhusu juisi au maji maji ya kwenye viazi yakae katika ngozi, na kisha baadae unaweza kuosha ngozi yako kwa maji ya vuguvugu, kwani viazi vina madini na vitamini ambazo zikinyonywa katika ngozi, husaidia kuondoa michirizi.

Mafuta ya Aloe vera, pakaa mafuta haya katika ngozi yenye michirizi, pia unaweza kuyachanganya na vitamini A na ukapakaa ngozi yako.

Katika ngozi yenye michirizi, pakaa juisi iliyotokana na malimao, limao linayo tindikali asilia, organic acid, ambayo husaidia kuponyesha makovu na michirizi ya ngozi.

Mpenzi msomaji, maji pia ni muhimu katika afya yako, maji husaidia kuondoa sumu mbalimbali mwilini kupitia ngozi na hivyo hukuwezesha kuwa na ngozi yenye afya zaidi.

Chanzo: Tanzlife Company Limited

 

 

 

 

 

About Admin

Avatar

Recommended for you

11 Comments