Articles

BAKTERIA WA MDOMONI KUTUMIKA KAMA ALAMA ZA VIDOLE (FINGERPRINTS)

By

on

KINYWA NA MENO

KINYWA NA MENO

Kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi katika chuo kikuu cha Ohio ( Ohio State University ) nchini Marekani, utafiti uliofanywa kwa watu wenye asili ya China, Wazungu, Walatino pamoja na watu wenye ngozi nyeusi wasiyokuwa Wahispania, wamegundua kuwa bakteria wanaopatikana katika fizi za mwanadamu hutofautiana.

Uchunguzi uliofanywa kwa vijidudu zaidi ya 400 vinavyopatikana katika kinywa cha mwanadamu, uliwawezesha watafiti hao kujua ni vijidudu vipi vimetoka kwa mchina, vipi kwa mlatino, mzungu na vipi vimetoka kwa mtu mweusi.

Matokeo hayo wanaamini yanaweza kuwa sawa na ambavyo alama za vidole, fingerprints, zinavyoweza kutumika kumtambua mtu asili yake ni ipi.

Awali wataalamu wa afya ya kinywa na meno waliamini kuwa, bakteria wote wasiyokuwa waharibifu (healthy bacteria) wanaopatikana katika kinywa cha binadamu wanafanana na hivyo kutoa matibabu ya kufanana kwa magonjwa mbalimbali ya kinywa. Lakini katika utafiti huo, wanasayansi hao wa chuo kikuu cha Ohio, hawakupata hata vinywa vya watu wawili vyenye kufanana, vyote vilitofautiana kwa aina ya bakteria.

Pia, kutokana na utafiti huo, imegundulika ni kwa nini baadhi ya magonjwa ya kinywa na meno ni rahisi kuwapata watu wa aina fulani au kundi fulani.

Utafiti huo uliotangazwa juma hili, umepongezwa na wanasayansi mbalimbali kwani wanaamini kuwa, utatoa mwongozo mzuri kwa madaktari wa kinywa na meno katika kutoa matibabu kwa wenye matatizo ya kinywa na meno, pia kutoa ukweli kwamba matibabu ya aina fulani kwa mgonjwa huyu, yanaweza yasimfae mgonjwa yule.

Bakteria hawa imeonekana kuwa, hutofautiana pia kutoka asili moja ya watu hadi nyingine (Human Races) na katika asili huenda kwa kurithi, hereditary bacteria, hivyo itawawezesha madaktari kuunda mifumo madhubuti ya kutoa matibabu.

Kukosekana kwa watu wanaofanana, japo wawili, hii imeelezwa kuwa sawa na alama za vidole, fingerprints.

Chanzo: Tanzlife Company Limited

 

 

 

About Admin

Avatar

Recommended for you