Articles

DAWA FEKI AU BANDIA

By

on

Kwa mujibu wa mamlaka ya chakula na dawa Tanzania, TFDA, dawa itakuwa bandia iwapo itakuwa na vigezo vifuatavyo:

Kwanza itakuwa imetengenezwa kwa jina lisilokuwa lake, mfano dawa ya Diclofenac ikapewa jina la Paracetamol. Pili ni kopo la dawa au chombo kilichotumika kuhifadhi dawa kuwa na jina la mtu au kampuni fulani inayodai kuwa mtengenezaji wa dawa hiyo lakini kiukweli mtu au kampuni hiyo haipo au haitambuliki. Tatu ni dawa kuonyesha kuwa imetengenezwa na kampuni fulani na kumbe siyo kweli. Nne ni dawa yote au kiasi cha dawa kuwa kimeondolewa na kufidiwa na dawa nyingine tofauti, na Tano au mwisho ni, dawa kuonyesha mfanano wa karibu sana na dawa nyingine bila ya kuwa na taarifa katika kopo zinazoonyesha jina halisi la dawa pamoja na taarifa muhimu za kuitofautisha dawa hiyo na dawa nyingine.

Mpenzi msomaji, lengo la mada hii pamoja na utangulizi huo hapo juu ni, kukumbushana na kubadilishana mawazo kuhusu mapambano dhidi ya vitu feki au bandia vinavyotumika katika jamii yetu.

Katika mada hii mpenzi msomaji, ni nini maoni yako kuhusu kupambana na dawa feki au bandia, jukumu hili ni la nani hasa?. Yawezekana ukawa umewahi kukutana na bidhaa au dawa bandia, na sidhani kama ungependa kuendelea kutumia bidhaa hizi, ni wewe ndiye msemaji mkuu katika mada hii, je, jukumu la kupambana na dawa bandia ni la nani?.

Tunawakaribisha wote katika kuchangia mada kupitia ukurasa huu sehemu ya maoni au comments, kupitia Health Forum katika website hii ya Tanzlife, kwa kutufuata katika Twitter account, @tanzlife, au kwa kupitia ukurasa wetu wa Facebook, Tanzlife.

TUNATANGULIZA SHUKURANI ZETU ZA DHATI KWENU

Chanzo: Tanzlife Company Limited

About Admin

Avatar

Recommended for you