Articles

DAWA YA VANCOMYCIN YAONEKANA KWA KUNGURU

By

on

KUNGURU

KUNGURU

Usugu wa vijidudu (Microbial Resistance) vinavyosababisha maambukizi ya magonjwa mbalimbali unazidi kuwa tatizo la kusikitisha kwa binadamu , tatizo hili linazidi kusambaa katika maeneo mengi zaidi kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya dawa (antibiotics) kwa binadamu na pia katika uzalishaji wa mifugo.

Utafiti mpya kutoka Chuo Kikuu cha mifugo nchini Marekani,Tufts, umeonyesha kwamba usugu wa vijidudu katika dawa unaenea kwa kiasi kikubwa na hivi sasa tatizo hili halipo tu hospitalini, bali lipo katika mashamba (mimea na mifugo) na pia katika mazingira ya asili wanakopatikana wanyamapori.

Kulingana na tafiti zilizofanywa kwa kukusanya sampuli mia sita ,600, za kinyesi cha ndege jamii ya kunguru kutoka katika maeneo tofauti tofauti, baada ya kuzifanyia uchunguzi waligundua kwamba, asilimia mbili na nusu ya ndege hao walikuwa na jeni (genes) zinazoonyesha usugu wa dawa ya Vancomycin, dawa ambayo inanguvu katika kupambana na visababishi mbalimbali vya magonjwa. Mbali na dawa ya Vancomycin, pia ulionekana usugu katika dawa nyingine ambazo zimekuwa zikitumiwa na binadamu katika kukuzia mifugo au kuwalisha mifugo.

Matokeo ya utafiti huu yanazidi kutia wasiwasi juu ya uwezo wa dawa mbalimbali katika kupambana na magonjwa na inazidi kuleta utata katika kupambana na tatizo la usugu wa vijidudu. Watafiti wanadhani kwamba, pia chanzo kinaweza kuwa ni sehemu zinakotupwa au kuharibiwa taka au maji taka yatokanayo na madawa na hivyo kupelekea ndege au wanyama kuzifikia taka hizo na kuzitumia na kusababisha tatizo hili kwa wanyama na baadae kulisambaza zaidi.

Utafiti huu unaonyesha kwamba kile ambacho binadamu anakifanya katika mazingira yake wenyewe  na katika mashamba ya mimea na mifugo, kinaathari kubwa katika mazingira yetu wanadamu na hata mazingira ya wanyamapori. Hivyo kunahaja ya kusimamia na kuboresha zaidi utumiaji wa madawa ili kulinda afya ya mwanadamu pamoja na viumbe wengine na kupunguza kasi ya kuenea kwa tatizo la usugu wa vijidudu katika dawa (Antimicrobial Resistance).

Chanzo: Tanzlife Company Limited

 

About Admin

Avatar

Recommended for you