Articles

FAIDA ZA KUTUMIA KITUNGUU SAUMU (GARLIC)

By

on

VITUNGUU SAUMU (GARLIC)

VITUNGUU SAUMU (GARLIC)

Katika mapishi watu tunayomazoea ya kutumia viungo mbalimbali ili kuongeza ladha katika chakula, moja ya kiungo ambacho kinatumiwa na watu wengi ni kitunguu saumu (garlic).

Kitunguu saumu katika chakula, pamoja na kuongeza ladha na harufu nzuri katika chakula, pia kinazo faida mbalimbali katika afya zetu, hii ni katika kuulinda mwili kwa kupambana na magonjwa mbalimbali. Kitunguu saumu hutupatia faida zifuatazo katika afya zetu:

Husaidia kupunguza tatizo la shinikizo la damu, (Reduce high blood pressure), katika mwili wa binadamu kuna protini (Angiotensin II) ambazo husababisha mishipa ya damu isinyae na hivyo kupelekea shinikizo kubwa la damu (high blood pressure), kemikali zilizopo ndani ya kitunguu saumu huzuia protini hizi zisisababishe mishipa ya damu kusinyaa na pia gesi ya hydrogen sulphide inayopatikana baada ya kemikali polysulphides (ipo katika kitunguu saumu) kuvunjwa katika chembe hai nyekundu za damu (red blood cells) husaidia kuifanya mishipa ya damu isisinyae (dilate) na hivyo kukuwezesha kuwa na shinikizo la damu la kawaida.

Huiwezesha damu kuwa nyepesi na kuepusha uwezekano wa damu kuganda na kusababisha mabonge mabonge ambayo ni hatari kwa afya yako, (blood thinning).

Huua vijimelea/vijidudu vinavyosababisha magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya ngozi, (antibacterial and antiviral properties). Pia imegundulika kwamba kwa kuweka kitunguu saumu katika chakula hupunguza uwezekano wa chakula kuharibika ( prevent food poisoning).

Kitunguu saumu huongeza uzalishaji wa insulin mwilini na hivyo kusaidia kuweka uwiano mzuri wa sukari katika mwili au damu, hivyo kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari huweza kupata msaada kwa kutumia kitunguu saumu.

Husaidia utayalishaji na utumiaji wa madini ya chuma mwilini, hii ni kwa kuongeza uzalishaji wa protini, Ferroportin, ambayo husaidia mwili kunyonya (absorption) madini ya chuma na hivyo kuboresha utumiaji wa madini (Iron) haya mwilini.

Hutibu matatizo ya meno, hii ni kutokana na kuwa na sifa ya kuuwa wadudu (antibacterial) na pia kuondoa maumivu (analgesic). Kata kipande kidogo cha kitunguu saumu na weka katika jino linalosumbua.

Husaidia kupunguza matatizo au magonjwa ya mfumo wa upumuaji, mfano koo kuwasha, pumu au kifua kubana. Kutokana na uwezo wake wa kusaidia watu wenye matatizo hayo, kitunguu saumu imekuwa kama dawa ya bei nafuu.

Kemikali zinazopatikana katika kitunguu saumu zimegundulika kusaidia kupungua hatari ya kupata kansa za aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na kansa za matiti (breast cancer), hivyo utumiaji wa kitunguu saumu huuwezesha mwili kuondoa sumu mbalimbali mwilini (Anti-oxidant).

Kitunguu saumu siyo tu kwamba hukifanya chakula kuwa kitamu na chenye harufu nzuri, ila pia kitunguu saumu ni dawa.

Chanzo: Tanzlife Company Limited

 

 

About Admin

Avatar

1 Comment