Articles

HERI YA MWAKA MPYA 2014

By

on

Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu pale mtu unapoweza kuiona siku mpya.

Ikiwa leo ni siku mpya na zaidi hasa ni siku ya kwanza ya mwaka mpya wa 2014, tunapenda kuwatakia heri ya mwaka mpya 2014. Mwaka huu mpya uwe ni wa mafanikio zaidi na mabadiliko chanya katika maisha yenu ya kila siku.

Pamoja na kuwatakia heri ya mwaka mpya, pia tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwenu kwa ushirikiano muliotupatia katika kipindi chote cha nyuma mpaka kutuwezesha kufika siku ya leo. TUNAWASHUKURU SANA.

Inawezekana kwa namna moja au nyingine tukawa tumemkwaza mtu kutokana na mapungufu yetu ya kibinadamu, tunawaomba ladhi na tupo tayari kujirekebisha pale tulipokosea.

Zaidi na zaidi, tunapenda kuwaahidi ya kuwa, tutaendelea kuwaletea elimu na dondoo mbalimbali za Afya, kuboresha namna ya kuwafikishia taarifa hizo lakini pia, tupo tayari muda na saa yoyote kusikiliza ushauri au maoni kutoka kwenu ili kazi hii iweze kuwa nzuri zaidi na watu wengi waweze kufaidika na kuishi wakiwa na Afya bora zaidi.

TUENDELEE KUWA PAMOJA NA MWENYEZI MUNGU AZIDI KUWABARIKI NA KUWAWEZESHA KUIONA MIAKA MINGINE MIPYA MINGI ZAIDI.

AHSANTENI SANA

HAPPY NEW YEAR 2014!!!

Chanzo: Tanzlife Company Limited

About Admin

Avatar