Articles

KUTOKUWA NA MUDA MAALUMU WA KULALA HUCHANGIA MTOTO KUWA NA MATATIZO YA TABIA

By

on

MTOTO KALALA

MTOTO KALALA

Jambo ambalo mtu mzima anaweza kushauriwa endapo anayo matatizo ya usingizi (kulala) ni kuwa na muda maalumu wa kulala, vivyo hivyo kwa watoto, ili waweze kuwa na uwezo wa kujitawala katika tabia zao na kuupatia ubongo uwezo wa kukua vizuri, wanahitaji wawe na muda maalumu na wa kutosha katika kulala.

Wazazi, waalimu pamoja na wataalamu wa afya, wanakubaliana na jambo hili kwamba, mtoto ambaye hana muda maalumu wa kulala huwa katika hatari zaidi ya kupata matatizo ya kitabia ikiwemo kulialia bila ya kuwa na sababu maalumu.

Sote tunafahamu kwamba, makuzi ya mtoto yanachangia kwa kiasi kikubwa namna afya yake itakavyokuwa pindi atakapokuwa mtu mzima, hivyo tatizo la kutokuwa na muda maalumu wa kulala akiwanalo wakati wa makuzi yake, itaathiri afya yake pia pindi atakapokuwa mtu mzima.

Mpenzi msomaji, miili yetu siku zote huwa inajizoesha katika utaratibu fulani ambao wewe binafsi unauweka, mfano, kama umejijengea utaratibu wa kuwa unaamka kila siku saa kumi na mbili asubuhi, basi mwili ukizoea hivyo itakuwa ni siku zote iko hivyo hata kama haujaiseti Alamu ikuamshe.

Kutokana na tabia hiyo ya miili yetu, endapo mtoto mdogo atakuwa hana muda au utaratibu maalumu wa kulala, itaathiri ukuaji wake wa mwili na ubongo kitu ambacho kiafya madhara yake yanaweza kuonekana akiwa bado mtoto na pia hata akiwa mtu mzima. Kama mtoto madhara yake kwa kutokuwa na muda maalumu wa kulala ni pamoja na, kulialia ovyo bila sababu, kuwa na ukorofi, kushindwa kujitawala katika kujisaidia mfano kukojoa na pia kuwa na matatizo yanayohusiana na hisia, jambo dogo tu lakini linaweza kumfanya awe na hisia tofauti na unavyotarajia.

Katika kuhakikisha kuwa watoto wetu wanakuwa katika afya iliyo nzuri, ukuaji wa kimwili, kiakiri na hata kiroho, ni jukumu la wazazi au walezi kulizingatia hili ili watoto wetu wakue vizuri.

Chanzo: Tanzlife Company Limited

 

About Admin

Avatar

Recommended for you

2 Comments