Articles

MATUMIZI YA DAWA ZA KIENYEJI SAMBAMBA NA DAWA ZA HOSPITALINI

By

on

Ndugu wapenzi na wafuatiliaji wa taarifa mbalimbali za mambo ya afya kupitia Blog yenu ya Tanzlife, ni matumaini yetu kuwa nyote mpo katika hali nzuri kiafya kwa uwezo wa muumba wetu.

Katika changamoto tunayopenda kuwashirikisha na kuwaomba mutoe maoni yenu siku ya leo, ni changamoto inayohusu matumizi ya dawa za kienyeji sambamba na dawa za hospitalini. Jambo hili ni miongoni mwa mambo ambayo yanatokea kila siku katika maswala yanayohusiana na afya, mgonjwa anapelekwa hospitalini, kulingana na hali yake Daktari anaona ni vyema mgonjwa alazwe ili apate uangalizi wa karibu kutoka kwa wataalamu wa afya, wakati mgonjwa anaendelea kupewa huduma hospitalini, inagundulika kuwa anatumia pia dawa za kienyeji ili kujitibu. Matumizi haya ya dawa za kienyeji sambamba na dawa za hospitalini yanatokea majumbani kwetu pia. Je, kwa mtazamo wako jambo hili unalionaje?.

Mpenzi msomaji kuwa huru kutoa maoni yako kupitia sehemu ya maoni katika Blog hii, kwa kupitia Health Forum katika Website hii, kwa njia ya Twitter @tanzlife, au kwa ku LIKE ukurasa wetu wa Facebook, Tanzlife, na kutoa maoni yako.

TUNATANGULIZA SHUKURANI ZETU ZA DHATI

Chanzo: Tanzlife Company Limited

About Admin

Avatar

Recommended for you