Articles

MATUMIZI YA MAJI TAKA KUMWAGILIA BUSTANI, JE NINI FAIDA NA HASARA ZAKE?

By

on

Mpenzi msomaji, ni siku nyingine tena ya kushirikishana na kubadilishana mawazo juu ya mambo yanayotendeka katika jamii yetu, na hasa mambo ambayo yanagusa afya zetu, kwani afya ni uhai, afya ni mtaji wa kufanya kila jambo. Hivyo hatuna budi kujua ni nini tunapaswa kukifanya ili tuendelee kuwa na afya nzuri.

Katika mada ya leo mpenzi msomaji, tuangalie kile ambacho kinafanyika katika bustani zetu, yawezekana zikawa ni bustani za mbogamboga, matunda au chochote kile ambacho kwa namna moja au nyingine kinagusa afya zetu kwa sisi kutumia mazao ya bustani hizo.

Bustani zilizo nyingi ambazo tunaziona maeneo ya mijini, zipo karibu au kwenye maeneo ya maji taka, mifereji inayopitisha maji machafu kutoka katika majumba ya watu au viwanda. Maji haya ndiyo yamekuwa yakitumika kumwagilia bustani, na sisi tumekuwa walaji wa mazao hayo ya bustani, swali ni je, nini faida au hasara za kutumia mazao hayo yaliyozalishwa kwa njia hiyo ya umwagiliaji, na pia kwa mkulima huyu ambaye muda mwingi anautumia akiwa katika maji hayo ambayo siyo salama, nini hatma ya afya yake?.

Mpenzi msomaji, karibu sana katika kuchangia mada hii, unaweza kutoa maoni yako kupitia ukurasa huu, sehemu ya maoni, kupitia Health Forum katika Website hii ya Tanzlife, kupitia ukurasa wetu wa Facebook, Tanzlife, au kupitia anwani yetu ya Twitter, @tanzlife.

Chanzo: Tanzlife Company Limited

About Admin

Avatar

Recommended for you