Articles

MISHIPA YA DAMU NA VALVU KUHARIBIKA (VARICOSE VEINS)

By

on

VARICOSE VEINS

VARICOSE VEINS

Tatizo linalofahamika kitaalamu kama, varicose veins, hutokea baada ya mishipa ya damu pamoja na valvu zinazoruhusu damu kusafiri upande mmoja kuharibika na hivyo kuifanya damu ijikusanye katika mishipa, na pindi inapojikusanya inakuwa nyingi na kupelekea mishipa itanuke zaidi na kufanya ionekane kama mizizi katika usawa wa ngozi.

Mara nyingi tatizo hili hutokea maeneo ya kwenye miguu na enka (ankles) ingawaje inaweza kutokea sehemu yoyote katika mwili.

Mpenzi msomaji, pamoja na tatizo hili kwenda kwa kurithi kuna mambo ambayo huwa yanapelekea mtu apate tatizo hili, na mambo hayo ni pampja na mtu kuwa na uzito mkubwa, ujauzito pamoja na mtu kutumia muda mwingi kusimama jambo ambalo linapelekea presha katika miguu iwe kubwa zaidi na hivyo kusababisha mishipa na valvu za damu katika miguu iharibike.

Dalili za mtu kuwa na tatizo hili ni pamoja na, kupata maumivu katika sehemu yenye tatizo (miguu), kubadilika rangi ya ngozi (dark blue), ngozi kuwasha, kuvimba  pamoja na muonekano au shape ya mishipa ya damu kubadilika ( kuwa kama mizizi katika usawa wa ngozi).

Tatizo hili linaweza kuwa ni dalili ya tatizo lingine katika mishipa yako ya damu, ambapo inawezekana mishipa ya ndani ya damu ikawa imeziba na hivyo kukusababishia matatizo mengine makubwa. Kitaalamu inaitwa deep vein thrombosis, itahitajika upasuaji au matibabu zaidi ya kitaalamu ili kuweza kupata msaada.

Mpenzi msomaji, kama sehemu ya tiba na huduma ya kwanza ukiwa unasubiri kuonana na mtaalamu wako wa afya, mambo ambayo unaweza kuyafanya ili kupunguza athari za tatizo hili ni pamoja na: Kuvaa soksi ndefu miguuni za kubana, kuepuka kusimama au kukaa kwa muda mrefu, kuinyanyua miguu endapo umekaa ili kupunguza presha katika miguu na kuwa unafanya mazoezi.

Hili ni tatizo ambalo kitaalamu linatibika, hivyo endapo unalo tatizo hili, usisite kuonana na wataalamu wa afya ili waweze kukusaidia na kukufanya muonekano wa ngozi yako au miguu iwe vizuri zaidi.

Chanzo: Tanzlife Company Limited

 

 

 

About Admin

Avatar

Recommended for you

3 Comments