Articles

MTOTO KUZALIWA MAPEMA (PREMATURE BABY)

By

on

MTOTO ALIYEZALIWA KAMLA YA MAJUMA 37

MTOTO ALIYEZALIWA KABLA YA MAJUMA 37

Kitendo cha mtoto kuzaliwa mapema au kwa lugha ya kitaalamu huitwa, Premature birth, hutokea pale ambapo mtoto anazaliwa kabla ya kufikisha majuma 37 (kabla hajafikisha miezi tisa akiwa tumboni mwa mama yake)

Mpenzi msomaji, tatizo hili la watoto kuzaliwa mapema hutokea kila siku na ni tatizo la dunia nzima, karibu watoto zaidi ya  milioni 14 huzaliwa kila mwaka duniani kote wakiwa hawajafikisha majuma 37 tumboni mwa mama zao.

Sababu zinazopelekea watoto kuzaliwa mapema kabla ya umri zipo tofauti tofauti, miongoni mwa sababu hizo ni kama vile, mama mjamzito kujihusisha na kazi ngumu, matumizi ya dawa au vinywaji ambavyo siyo salama kwa mama mjamzito, kuwa mjamzito katika umri mkubwa, matatizo katika shingo ya kizazi na hivyo mwanamke kushindwa kustahimili ujauzito, kuugua sana wakati mwanamke akiwa mjamzito na sababu nyingine nyingi.

Baada ya kuzaliwa, watoto hawa ambao wamezaliwa mapema hukumbwa na matatizo au changamoto mbalimbali za kiafya, miongoni mwa matatizo ya kiafya wanayoyapata ni pamoja na: Matatizo katika neva za fahamu, matatizo katika mfumo wa upumuaji (mapafu kushindwa kutanuka na kusinyaa wakati wa upumuaji kutokana na kukosekana kwa protini maalumu, surfactant, katika mapafu), kupata matatizo ya damu na homa ya manjano kutokana na Ini kutokukomaa vizuri, matatizo katika uwezo wa kuona pamoja na hatari ya kupata magonjwa ya kuambukizwa kwa kirahisi. Matatizo haya huweza kuwaathiri watoto hawa kwa muda wa maisha yao yote.

Mpenzi msomaji, ni jukumu la kila mmoja wetu kuchukua tahadhari ili kupunguza au kuepukana na tatizo hili la watoto kuzaliwa mapema, kama mama mjamzito ni wajibu wako kuhakikisha kuwa unafuata maelekezo unayopewa na wataalamu wa afya kwa usalama wako na wa mwanao pia, na jamii kwa ujumla ni vizuri tukaendelea kukumbushana juu ya umuhimu wa akina mama wajawazito kwenda kliniki ili wapewe elimu ya afya itakayowawezesha kuishi na kuja kujifungua salama na katika muda muafaka.

Chanzo: Tanzlife Company Limited

 

 

 

About Admin

Avatar

Recommended for you