Articles

NGOZI YAKO

By

on

KUITUNZA NGOZI

KUITUNZA NGOZI

Ngozi huchangia asilimia sita mpaka kumi (6% – 10%) ya uzito wa mwili wa binadamu na pia ina ukubwa wa wastani wa futi za mraba ishirini na moja kwa mtu mzima.Hii hupelekea ngozi kuwa ni kiungo ambacho ni kikubwa katika mwili wa mwanadamu.

Katika mwili wa binadamu, ngozi hufanya kazi mbalimbali na miongoni mwa kazi hizo ni kama vile:- kurekebisha joto la mwili, kutoa taka mwilini, njia ya kumpatia mtu matibabu (dawa za kupakaa, dawa za sindano) na pia ngozi huvilinda/huvifunika viungo vingine katika mwili.

Ili ngozi iweze kufanya kazi zake vizuri, inahitaji ipewe matunzo mazuri. Miongoni mwa matunzo ya ngozi hujumuisha usafi, ulaji wa chakula chenye virutubisho (Vitamins huimarisha ngozi), kunywa maji ya kutosha (sumu mbalimbali hutoka mwilini kwa njia ya jasho) na pia utumiaji wa mafuta ya kupakaa na losheni huchangia katika kuitunza ngozi.

Mara nyingi tumekuwa tukiona au hata kututokea sisi wenyewe katika miili yetu, baada ya kutumia mafuta Fulani au losheni Fulani, ngozi yako ikapata mabadiliko ambayo hukuyategemea, badala ya ngozi yako kulainika, ikawa ya kukakamaa, au badala ya kuifanya ngozi iwe na afya, ikawa na chunusi au vijipele. Miongoni mwa sababu zinazochangia matatizo haya ni utumiaji wa mafuta/losheni ambazo haziendani na aina ya ngozi tulizonazo.

Kabla ya mtu kuamua kutumia losheni/mafuta Fulani ya kupakaa ngozi yako, ni vyema ukaifahamu ngozi yako ni ya namna gani, mfano je ni ya asili ya mafuta mengi, au ni ya asili ya ukavu bila ya kuwa na mafuta mengi?, ili kuweza kujifahamu unaweza kufanya zoezi hili dogo, andaa karatasi nyeupe yenye ukubwa wa kutosha kuufunika uso wako, na kisha asubuhi unapoamka kabla ya kufanya kitu chochote ufunike uso wako kwa karatasi hiyo kwa muda wa dakika mbili hadi tatu, kisha itoe karatasi na iangalie, kama ngozi yako ni ya asili ya mafuta mengi, karatasi itakuwa na alama za mafuta, lakini kama hautaona alama hizo inamaana ngozi yako haina asili ya mafuta, unaweza kutumia njia hiyo au nyingine ili kuifahamu asili ya ngozi yako. Hii itakuwezesha kujua ni aina gani ya mafuta/losheni au kipodozi kinachokufaa kutumia kwa kutegemeana na aina ya ngozi uliyonayo.

Baada ya kuwa umeifahamu asili ya ngozi yako na aina ya mafuta au losheni unayopaswa kutumia, ni muhimu kutumia mafuta hayo au losheni katika muda unaofaa, mfano, kiafya tunashauriwa kuwa, wakati wa usiku tunapolala, tusiupakae mwili mafuta ili kuipa ngozi nafasi ya vinyweleo kuwa wazi zaidi na pia ngozi ipate hewa ya kutosha na itoe taka mwilini.

Ni vyema tukatumia vitu/vipodozi vinavyoendana na ngozi zetu au tupate ushauri kutoka kwa wataalamu ili tuweze kupunguza matatizo ya ngozi kama vile chunusi, vijipele na majipu.

Chanzo: Tanzlife Company Limited

About Admin

Avatar

Recommended for you

11 Comments